TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA UALIMU
UTANGULIZI
Shule ya Sekondari GOD’S BRIDGE ni kati ya shule zinazomilikiwa na kuendeshwa na God’s Bridge Development Foundation Co. Ltd. Shule inaendeshwa kwa misingi ya imani ya Kanisa la Waadventista Wasabato, ikiwa na wanafunzi kuanzia Kidato cha I hadi cha VI.
Shule ipo Km 6 kutoka Barabara Kuu ya Mbeya–Malawi, karibu na KKK Jirani na Chuo cha Magereza Kiwira.
NAFASI ZA KAZI
Uongozi wa Shule ya Sekondari GOD’S BRIDGE unawatangazia nafasi za kazi ya ualimu katika masomo yafuatayo:
PHYSICS (FIZIKIA) – Nafasi 01 (O-Level & A-Level)
ENGLISH (KIINGEREZA) – Nafasi 01 (O-Level & A-Level)
GEOGRAPHY (JIOGRAFIA) – Nafasi 01 (O-Level & A-Level)
KISWAHILI – Nafasi 01 (O-Level & A-Level)
SIFA ZA MUOMBAJI NA MAANDALIZI ANAYOTAKIWA KUYAFANYA
Mwombaji anatakiwa kuwa na:
Elimu ya ngazi ya Shahada ya Ualimu katika somo husika
Barua ya Maombi
Vyeti halisi pamoja na vivuli vyake
Wasifu Binafsi (CV)
Uwezo wa kuandika (kutakuwa na mtihani)
Mpango wa somo la kufundishia (Lesson Plan)
USAILI
Usaili utafanyika katika Shule ya Sekondari GOD’S BRIDGE – Tukuyu.
Muda wa usaili utaanza saa 2:00 asubuhi kulingana na ratiba ifuatayo:
RATIBA YA USAILI
| Siku/Tarehe | Somo |
|---|---|
| Jumanne, 13/01/2026 | Physics (Fizikia) |
| English (Kiingereza) | |
| Geography (Jiografia) | |
| Kiswahili |
Imetolewa na:
MUSA LUSATO
MKUU WA SHULE
Tarehe: 28/12/2025
