Find Your Dream Job Today

NECTA KISWAHILI PAST PAPER 2025 NA MAJIBU

Deadline: Checking...
Posted on Monday, 9 February 2026 Loading
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
MTIHANI WA KUHITIMU KIDATO CHA NNE
2025

021 KISWAHILI
(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)
Maelekezo:
1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) kutoka sehemu C ambapo swali la tisa (9) ni la lazima.
3. Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30).
4. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
5. Muda Allowed: Saa 3
SEHEMU A (Alama 16)
1.
Katika vipengele (i) hadi (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia.
(i) Ni taarifa zipi zinaweza kupatikana katika kamusi kati ya hizi?
A. Neno, maana, matamshi na matumizi ya semi B. Maana, neno, mazungumzo na matumizi ya semi C. Matumizi ya semi, matamshi, maana na mazungumzo D. Matamshi, mazungumzo, maana na kidahizo E. Kidahizo, matamshi, mazungumzo na semi
(ii) "Juma anaendesha baiskeli yake polepole." Kiarifu cha sentensi hii kimejengwa na mfuatano upi wa vipashio?
A. Kiima, chagizo na shamirisho B. Kitenzi kishirikishi, shamirisho na chagizo C. Kiarifu, kiima na chagizo D. Shamirisho, chagizo na kitenzi kikuu E. Kitenzi kikuu, shamirisho na chagizo
(iii) "Tutakuja kumpokea kwenye uwanja wa ndege." Kazi ya kielezi kinachojitokeza kwenye sentensi hii ni ipi kati ya hizi?
A. Kueleza idadi B. Kueleza mahali C. Kueleza namna D. Kueleza wakati E. Kueleza nafsi
(iv) Tamathali ipi ya semi hufananisha mambo kwa kutumia viunganishi?
A. Tashititi B. Sitiari C. Nidaa D. Tashibiha E. Tabaini
(v) Tamathali ipi ya semi inatawala katika wimbo ufuatao?
Ze ndi ndi ndi!
Tolly ndi!
Ndi ndi ndi ndi!
Tolly ndi! x4
A. Tabaini B. Taniaba C. Tashibiha D. Takriri E. Tashihisi
(vi) Neno lipi linadhihirisha kauli ya kutendeka katika kitenzi pika?
A. Pikia B. Pikiwa C. Pikika D. Pikwa E. Pikisha
(vii) Yupi kati ya wafuatao anajishughulisha na kusoma, kuchambua na kutoa maoni katika kazi za sanaa?
A. Mdhamini B. Mtunzi C. Mhariri D. Msomaji E. Mhakiki
(viii) Hatua mojawapo ya uendelezaji wa lugha ili itumike kitaifa na kimataifa ni kuisanifisha. Jambo lipi kubwa linalofanywa katika hatua hii kati ya yafuatayo?
A. Kupunguza maneno ya kukopa B. Kuondoa tofauti za kimsamiati C. Kuifanya itumike na jamii ndogo D. Kuweka tofauti za matamshi E. Kuidhinisha tofauti za maneno
(ix) Ni kwa namna gani tungo hutofautiana na sentensi?
A. Tungo zote ni sentensi lakini sentensi zote si tungo B. Sentensi haitoi taarifa kamili lakini tungo hutoa taarifa kamili C. Sentensi ni miongoni mwa tungo lakini si kila tungo ni sentensi D. Tungo sharti ikamilike lakini sentensi si lazima ikamilike E. Tungo ni ndefu sana lakini sentensi ni fupi sana
(x) Jambo lipi si muhimu katika uandishi wa kadi ya mwaliko?
A. Jina la mwandishi na mwalikwa B. Idadi ya waalikwa C. Tarehe ya tukio D. Kusudi la tukio E. Mahali tukio linapofanyika
2.
Oanisha mifano ya tamathali za semi iliyo katika Orodha A na tamathali husika zilizo katika Orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.
Orodha AOrodha B
(i) Kilio cha mama mfiwa kilisikika mithili ya king'ora.A. Mjalizo
(ii) Haba na haba hujaza kibaba.B. Tashihisi
(iii) Misitu ni uhai.C. Tasfida
(iv) Shangazi amejifungua salama.D. Tabaini
(v) Upepo mkali ulipiga miluzi kila ulipogonga kingo za mito.E. Tashibiha
(vi) Binadamu hupanga, Mungu hupangua.F. Onamatopea
G. Sitiari
H. Takriri
SEHEMU B (Alama 54)
3.
(a) Tumia mzizi chez- kuunda vitenzi viwili kwa kila kauli kama zilivyoorodheshwa:
   (i) Kauli ya kutendeana
   (ii) Kauli ya kutendana
   (iii) Kauli ya kutendeka
   (iv) Kauli ya kutendewa
(b) Unda nomino moja kwa kila kitenzi:
   (i) Zaa (ii) Kimbia (iii) Shikilia (iv) Elekeza (v) Penda
4.
(a) Fafanua vyanzo vinne vya misimu kwa kutoa mfano mmoja kwa kila chanzo cha msimu husika.
(b) Eleza maana mbili kwa kila neno:
   (i) Kaka (ii) Kito (iii) Mkaa (iv) Mkwaju (v) Babu
5.
Bainisha viambishi vya o-rejeshi katika kila sentensi kwa kuvipigia mstari kisha taja ngeli husika kwa kila kirejeshi.
(a) Udongo ulioleta umekauka
(b) Kioo kilichovunjika kimeletwa
(c) Karatasi zilizokauka zimetumika
(d) Mlimokuwa mna joto sana
(e) Kijana atakayeshinda atapewa zawadi
(f) Gazeti lililochapwa limekwisha
(g) Barabara iliyofunguliwa imekamilika
(h) Magonjwa yaliyowasumbua yalitokana na athari ya mvua
(i) Ng'ombe aliyeangukia shimoni ameokolewa
6.
Eleza kwa kifupi maana ya nahau zifuatazo:
(a) Juma ana mkono wa birika (b) Kaka amepata jiko (c) Mjomba amepiga maji (d) Mwizi amekata mguu (e) Mtoto amevimba kichwa (f) Beka ana mkono mrefu (g) Rafiki yangu anakaza kamba (h) Kijana amepiga kete (i) Huyu ana damu mbichi
7.
Eleza kwa kifupi sifa sita zilizokifanya Kiunguja kusanifishwa na kuwa lugha sanifu ya Kiswahili.
8.
Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata:

"Kwa hakika mwaka ule watu walivuna sana. Haikuwahi kutokea takribani kwa kipindi cha muongo mmoja hivi kuwa na mavuno kiasi hicho. Maghala yalijaa mahindi, mtama, mpunga, uwele, mbaazi, maharage, njegere na njugumawe. Nyama nyingi ililetwa kutoka porini ambapo wanawake walizitanda na kuzikausha motoni. Aidha, samaki wakubwawakubwa walipatikana kwa wingi, samaki ambao hawakuwahi kupatikana hapo awali. Kila mmoja kijijini hapo alikuwa na furaha..."

Maswali:
(a) Andika kichwa cha habari uliyoisoma kisichopungua maneno matatu na kisichozidi maneno matano.
(b) Bainisha shughuli mbili muhimu zilizokuwa zikiwapatia watu riziki kulingana na habari uliyosoma.
(c) Fafanua kwa kifupi maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika habari uliyoisoma: (i) Muongo mmoja (ii) Waliwapiku
(d) Fupisha habari hii kwa maneno yasiyopungua mia moja (100) na yasiyozidi mia na tano (105).
SEHEMU C (Alama 30)
9.
Jifanye wewe ni mmojawapo wa watoto waliohudhuria kongamano lililohusu haki za watoto. Andika beti tano za utenzi kuhusu "Haki za Mtoto."
10.
Lengo kuu la kazi za fasihi ni kuonya na kuiasa jamii. Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila riwaya kutoka katika riwaya mbili ulizosoma kati ya hizi:
Takadini - Ben J. Hanson, Watoto wa Mama N'tilie - E. Mbogo, Joka la Mdimu - A. J. Safari.
11.
"Uzembe ni jambo linalokwamisha maendeleo ya jamii nchini Tanzania." Tathmini kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila tamthiliya kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma kati ya hizi:
Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe - E. Semzaba, Kilio Chetu - Medical Aid Foundation.

MARKING SCHEME HERE